Kum. 33:18-24 Swahili Union Version (SUV)

18. Na Zabuloni akamnena,Furahi Zabuloni, katika kutoka kwako;Na Isakari, katika hema zako.

19. Watayaita mataifa waje mlimani;Wakasongeze huko sadaka za haki;Kwa kuwa watanyonya wingi wa bahari,Na akiba zilizofichamana za mchangani.

20. Na Gadi akamnena,Na abarikiwe amwongezaye Gadi;Yeye hukaa kama simba mke,Hurarua mkono, naam, na utosi wa kichwa.

21. Akajichagulia sehemu ya kwanza,Kwani ndiko lilikowekwa fungu la mtoa-sheria;Akaja pamoja na wakuu wa watu,Akaitekeleza haki ya BWANA,Na hukumu zake kwa Israeli.

22. Na Dani akamnena,Dani ni mwana-simba,Arukaye kutoka Bashani.

23. Na Naftali akamnena,Ee Naftali, uliyeshiba fadhili,Uliyejawa na baraka ya BWANA;Umiliki magharibi na kusini.

24. Na Asheri akamnena,Na abarikiwe Asheri kwa watoto;Na akubaliwe katika nduguze,Na achovye mguu wake katika mafuta.

Kum. 33