17. Mzaliwa wa kwanza wa ng’ombe wake mume, enzi ni yake;Na pembe zake ni pembe za nyati;Kwa hizo atayasukuma mataifa yote, hata ncha za nchi;Nao ni makumi ya maelfu ya Efraimu,Nao ni maelfu ya Manase.
18. Na Zabuloni akamnena,Furahi Zabuloni, katika kutoka kwako;Na Isakari, katika hema zako.
19. Watayaita mataifa waje mlimani;Wakasongeze huko sadaka za haki;Kwa kuwa watanyonya wingi wa bahari,Na akiba zilizofichamana za mchangani.
20. Na Gadi akamnena,Na abarikiwe amwongezaye Gadi;Yeye hukaa kama simba mke,Hurarua mkono, naam, na utosi wa kichwa.
21. Akajichagulia sehemu ya kwanza,Kwani ndiko lilikowekwa fungu la mtoa-sheria;Akaja pamoja na wakuu wa watu,Akaitekeleza haki ya BWANA,Na hukumu zake kwa Israeli.