8. Yeye Aliye Juu alipowapa mataifa urithi wao,Alipowabagua wanadamu,Aliweka mipaka ya watuKwa kadiri ya hesabu ya wana wa Israeli.
9. Maana, sehemu ya BWANA ni watu wake,Yakobo ni kura ya urithi wake.
10. Alimkuta katika nchi ya ukame,Na katika jangwa tupu litishalo;Alimzunguka, akamtunza;Akamhifadhi kama mboni ya jicho;
11. Mfano wa tai ataharikishaye kioto chake;Na kupapatika juu ya makinda yake,Alikunjua mbawa zake, akawatwaa,Akawachukua juu ya mbawa zake;
12. BWANA peke yake alimwongoza,Wala hapakuwa na mungu mgeni pamoja naye.