Kum. 32:1-6 Swahili Union Version (SUV)

1. Sikilizeni, enyi mbingu, nami nitanena;Na nchi isikie maneno ya kinywa changu.

2. Mafundisho yangu yatadondoka kama mvua,Maneno yangu yatatona-tona kama umande;Kama manyunyu juu ya majani mabichi;Kama matone ya mvua juu ya mimea.

3. Maana nitalitangaza Jina la BWANA;Mpeni ukuu Mungu wetu.

4. Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu;Maana, njia zake zote ni haki.Mungu wa uaminifu, asiye na uovu,Yeye ndiye mwenye haki na adili.

5. Wametenda mambo ya uharibifu,Hawawi watoto wake, hii ndiyo ila yao;Wao ni kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka.

6. Je! Mnamlipa BWANA hivi,Enyi watu wapumbavu na ujinga?Je! Yeye siye baba yako aliyekununua?Amekufanya, na kukuweka imara.

Kum. 32