Kum. 28:59-63 Swahili Union Version (SUV)

59. ndipo atakapofanya BWANA mapigo yako yawe ya ajabu, na mapigo ya uzao wako, mapigo makubwa kwa kweli, ya kudumu sana, na magonjwa mazito ya kudumu sana.

60. Naye atakurejezea maradhi yote ya Misri juu yako uliyokuwa ukiyaogopa, nayo yataambatana nawe.

61. Tena kila ugonjwa, na kila pigo yasiyoandikwa katika kitabu cha torati hii, atakutia nayo BWANA juu yako, hata utakapokwisha kuangamizwa.

62. Nanyi mtasalia wachache kwa hesabu, ninyi mliokuwa mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi; kwa kuwa hukuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako.

63. Tena itakuwa, kama vile alivyokuwa akifurahi BWANA juu yenu kwa kuwatendea mema na kuwafanya kuwa wengi, ndivyo atakavyofurahi BWANA juu yenu kwa kuwapoteza na kuwaangamiza; nanyi mtanyakuliwa katika hiyo nchi mwingiayo kuimiliki.

Kum. 28