7. ufanye na sadaka za amani, ukale huko; nawe furahi mbele za BWANA, Mungu wako.
8. Kisha, andika juu ya mawe hayo maneno ya torati hii yote, waziwazi sana.
9. Musa na makuhani Walawi wakawaambia Israeli wote wakasema, Nyamaza, usikize, Ee Israeli; leo umekuwa watu wa BWANA, Mungu wako.
10. Basi isikize sauti ya BWANA, Mungu wako, ufanye maagizo yake na amri zake nikuagizavyo leo.
11. Musa akawaagiza wale watu siku iyo hiyo, akasema,
12. Hawa na wasimame juu ya mlima wa Gerizimu kwa kuwabarikia watu, mkiisha vuka Yordani; Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Yusufu, na Benyamini;
13. na hawa na wasimame juu ya mlima wa Ebali kwa laana; Reubeni, na Gadi, na Asheri, na Zabuloni, na Dani, na Naftali.
14. Kisha Walawi na wajibu, wawaambie watu wote wa Israeli kwa sauti kuu,