15. Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa BWANA, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina.
16. Na alaaniwe amdharauye baba yake au mama yake. Na watu wote waseme, Amina.
17. Na alaaniwe aondoaye mpaka wa jirani yake. Na watu wote waseme, Amina.
18. Na alaaniwe ampotezaye kipofu akakosa njia. Na watu wote waseme, Amina.
19. Na alaaniwe apotoaye hukumu ya mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe. Na watu wote waseme, Amina.
20. Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa kuwa amefunua mavazi ya babaye. Na watu wote waseme, Amina.