Kum. 25:14-17 Swahili Union Version (SUV)

14. Usiwe na vipimo mbalimbali, kikubwa na kidogo, katika nyumba yako.

15. Uwe na jiwe timilifu la haki, uwe na kipimo kitimilifu cha haki; zipate kuwa nyingi siku zako, katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako.

16. Kwa kuwa wote wayatendao mambo kama haya, wote watendao yasiyo haki, ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako.

17. Kumbuka aliyokufanya Amaleki katika njia mlipokuwa mkitoka Misri;

Kum. 25