1. Aonekanapo mtu ameuawa katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako, kuimiliki, amelala kondeni, wala haijulikani ni nani aliyempiga;
2. na watoke nje wazee wako na waamuzi wako, nao wapime hapo mpaka miji iliyomzunguka huyo aliyeuawa;
3. na iwe, mji ulio karibu na yule aliyeuawa, wale wazee wake mji huo watwae mtamba katika kundi la ng’ombe, ambaye hajafanya kazi, wala hajakokota jembe la nira;
4. wazee wa mji huo na wamshushe yule mtamba mpaka bonde lenye maji ya mtoni, lisilolimwa wala kupandwa, wakamvunje yule mtamba shingo yake humo bondeni;