27. Nipishe katikati ya nchi yako; nitakwenda kwa njia ya barabara, sitageuka kwenda mkono wa kuume wala wa kushoto.
28. Nawe uniuzie chakula kwa fedha nile; unipe na maji kwa fedha, ninywe; ila unipishe katikati kwa miguu yangu, hayo tu;
29. kama walivyonifanyia hao wana wa Esau waketio Seiri, na hao Wamoabi waketio Ari; hata nivuke Yordani niingie nchi tupewayo na BWANA, Mungu wetu.
30. Lakini Sihoni mfalme wa Heshboni hakutuacha kupitia kwake; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, alimfanya mgumu roho yake, akamtia ukaidi moyoni mwake, apate mtia mkononi mwako kama alivyo hivi leo.
31. Kisha BWANA akaniambia, Tazama, nimeanza kumtoa Sihoni na nchi yake mbele yako; anza kuimiliki, upate kuirithi nchi yake.
32. Ndipo Sihoni alipotutokea juu yetu yeye na watu wake wote, kupigana huko Yahasa.
33. BWANA, Mungu wetu, akamtoa mbele yetu, tukampiga yeye na wanawe, na watu wake wote.
34. Tukatwaa miji yake yote wakati huo, tukaharibu kabisa kila mji uliokuwa na watu, pamoja na wanawake na wadogo; tusimsaze hata mmoja;
35. ila ng’ombe zao tuliwatwaa kuwa mawindo yetu, pamoja na nyara za miji tuliyoitwaa.
36. Kutoka Aroeri iliyo katika ukingo wa bonde la Arnoni, na huo mji ulio ndani ya bonde, mpaka kufika Gileadi, hapakuwa na mji uliokuwa mrefu kutushinda; BWANA, Mungu wetu, aliiweka wazi yote mbele yetu; ila nchi ya wana wa Amoni hukuisongelea;
37. upande wote wa mto wa Yaboki, na miji ya nchi ile ya milimani, na kila mahali alipotukataza BWANA, Mungu wetu.