Kum. 17:1-6 Swahili Union Version (SUV)

1. Usimchinjie BWANA, Mungu wako, ng’ombe wala kondoo aliye na kilema, wala neno ovu lo lote; kwa kuwa hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako.

2. Ikiwa ameonekana katikati yako, ndani ya malango yako mojawapo, upewayo na BWANA, Mungu wako, mtu mume au mke afanyaye yaliyo maovu machoni pa BWANA, Mungu wako, kwa kuvunja maagano yake,

3. naye amekwenda kutumikia miungu mingine na kuiabudu, au jua, au mwezi, au vilivyo katika jeshi la mbinguni vyo vyote, nisivyoagiza mimi;

4. ukiambiwa hayo nawe umeyasikia, ndipo utafute kwa bidii, na tazama, ikiwa ni kweli lina hakika jambo lile, kuwa yafanywa machukizo kama hayo katika Israeli;

5. ndipo umchukue nje malangoni kwako, yule mtu mume, au yule mwanamke, aliyefanya jambo lile ovu; ukawapige kwa mawe, wafe.

6. Huyo atakayeuawa na auawe kwa midomo ya mashahidi wawili, au mashahidi watatu; asiuawe kwa mdomo wa shahidi mmoja. Ebr 10:28

Kum. 17