8. na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.
9. Mtakula hawa katika wote walio majini; kila kilicho na mapezi na magamba mtakula;
10. na kila kisichokuwa na mapezi na magamba msile; ni najisi kwenu.
11. Mna ruhusa kula katika nyuni wote walio safi.
12. Lakini hawa msiwale; tai, na furukombe, na kipungu;
13. na kengewa, na kozi, na mwewe kwa aina zake;
14. na kila kunguru kwa aina zake;
15. na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake;
16. na bundi, na mumbi, na bundi mkubwa;
17. na mwari, na nderi, na mnandi;
18. na membe, na koikoi, kwa aina zake; na hudihudi, na popo.
19. Na wadudu wote watambaao wenye mabawa ni najisi kwenu; msiwale.