Kum. 14:7-17 Swahili Union Version (SUV)

7. Lakini, hawa msile katika wale wenye kucheua, na hao waliopasuliwa ukwato; ngamia, na sungura, na kwang’a, kwa kuwa hucheua, lakini hawakupasuliwa kwato, ni najisi kwenu;

8. na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.

9. Mtakula hawa katika wote walio majini; kila kilicho na mapezi na magamba mtakula;

10. na kila kisichokuwa na mapezi na magamba msile; ni najisi kwenu.

11. Mna ruhusa kula katika nyuni wote walio safi.

12. Lakini hawa msiwale; tai, na furukombe, na kipungu;

13. na kengewa, na kozi, na mwewe kwa aina zake;

14. na kila kunguru kwa aina zake;

15. na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake;

16. na bundi, na mumbi, na bundi mkubwa;

17. na mwari, na nderi, na mnandi;

Kum. 14