3. Usile kitu cho chote kichukizacho.
4. Wanyama mtakaokula ni hawa ng’ombe, na kondoo, na mbuzi,
5. kulungu, na paa, na kongoni, na mbuzi wa mwitu, na paa mweupe, na pofu, na mbuzi wa mlima;
6. na kila mnyama aliyepasuliwa ukwato, ukapasuka ukwato wake zikawa mbili, naye ni mnyama mwenye kucheua akatafuna tena, katika wanyama wote, ndiye mnyama mtakayemla.
7. Lakini, hawa msile katika wale wenye kucheua, na hao waliopasuliwa ukwato; ngamia, na sungura, na kwang’a, kwa kuwa hucheua, lakini hawakupasuliwa kwato, ni najisi kwenu;
8. na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.
9. Mtakula hawa katika wote walio majini; kila kilicho na mapezi na magamba mtakula;
10. na kila kisichokuwa na mapezi na magamba msile; ni najisi kwenu.
11. Mna ruhusa kula katika nyuni wote walio safi.
12. Lakini hawa msiwale; tai, na furukombe, na kipungu;
13. na kengewa, na kozi, na mwewe kwa aina zake;
14. na kila kunguru kwa aina zake;