Kum. 14:26-28 Swahili Union Version (SUV)

26. na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng’ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za BWANA, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako;

27. na Mlawi aliye ndani ya malango yako usimwache, kwani hana fungu wala urithi pamoja nawe.

28. Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako;

Kum. 14