Kum. 14:1-9 Swahili Union Version (SUV)

1. Ninyi mmekuwa wana wa BWANA, Mungu wenu; msijitoje miili yenu, wala msifanye upaa katikati ya macho yenu kwa ajili ya aliyekufa.

2. Kwa kuwa u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako, na BWANA amekuchagua kuwa watu wake hasa, kuliko mataifa yote yaliyo juu ya uso wa nchi.

3. Usile kitu cho chote kichukizacho.

4. Wanyama mtakaokula ni hawa ng’ombe, na kondoo, na mbuzi,

5. kulungu, na paa, na kongoni, na mbuzi wa mwitu, na paa mweupe, na pofu, na mbuzi wa mlima;

6. na kila mnyama aliyepasuliwa ukwato, ukapasuka ukwato wake zikawa mbili, naye ni mnyama mwenye kucheua akatafuna tena, katika wanyama wote, ndiye mnyama mtakayemla.

7. Lakini, hawa msile katika wale wenye kucheua, na hao waliopasuliwa ukwato; ngamia, na sungura, na kwang’a, kwa kuwa hucheua, lakini hawakupasuliwa kwato, ni najisi kwenu;

8. na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.

9. Mtakula hawa katika wote walio majini; kila kilicho na mapezi na magamba mtakula;

Kum. 14