30. Je! Haiwi ng’ambo ya Yordani? Nyuma ya njia ya machweo ya jua, katika nchi ya Wakanaani waketio katika Araba kuelekea Gilgali, kando ya hiyo mialoni ya More?
31. Kwani ninyi mtavuka Yordani mwingie kuimiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wenu, nanyi muimiliki na kuketi humo.
32. Nanyi angalieni mzifanye amri na hukumu zote niwawekeazo leo mbele yenu.