Kum. 10:19-22 Swahili Union Version (SUV)

19. Basi, mpendeni mgeni, kwa sababu ninyi wenyewe mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.

20. Mche BWANA, Mungu wako, umtumikie yeye; ambatana naye, na kuapa kwa jina lake.

21. Yeye ndiye fahari yako, na yeye ndiye Mungu wako, aliyekutendea mambo haya makubwa, ya kutisha, uliyoyaona kwa macho yako.

22. Baba zako walishukia Misri na watu sabini; na sasa BWANA, Mungu wako, amekufanya kama nyota za mbinguni kwa wingi.

Kum. 10