Kol. 3:4-8 Swahili Union Version (SUV)

4. Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu.

5. Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;

6. kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu.

7. Katika hayo ninyi nanyi mlitembea zamani, mlipoishi katika hayo.

8. Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu.

Kol. 3