7. Maongeo ya enzi yake na amaniHayatakuwa na mwisho kamwe,Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake;Kuuthibitisha na kuutegemezaKwa hukumu na kwa haki,Tangu sasa na hata milele.Wivu wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo.
8. Bwana alimpelekea Yakobo neno, likamfikilia Israeli.
9. Nao watu wote watajua, yaani, Efraimu na yeye akaaye Samaria, wasemao kwa kiburi na kwa kujisifu nafsi zao,
10. Matofali yameanguka, lakini sisi tutajenga kwa mawe yaliyochongwa; mikuyu imekatwa lakini sisi tutaweka mierezi badala yake.
11. Kwa sababu hiyo BWANA atawainua adui wa Resini juu yake, naye atawachochea adui zake;
12. Waashuri upande wa mbele, na Wafilisti upande wa nyuma, nao watamla Israeli kwa kinywa kilicho wazi. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.
13. Lakini watu hao hawakumwelekea yeye aliyewapiga, wala kumtafuta BWANA wa majeshi.
14. Kwa sababu hiyo BWANA atakata katika Israeli kichwa na mkia, kuti na nyasi, katika siku moja.
15. Mzee mwenye kuheshimiwa ndiye kichwa, na nabii afundishaye uongo ndiye mkia.
16. Kwa maana wawaongozao watu hawa ndio wawakoseshao, na hao walioongozwa na watu hao wameangamia.