5. Maana silaha zote za mtu mwenye silaha wakati wa mshindo, na mavazi yaliyofingirishwa katika damu, yatakuwa tayari kuteketezwa, yatakuwa kuni za kutiwa motoni.
6. Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,Tumepewa mtoto mwanamume;Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;Naye ataitwa jina lake,Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu,Baba wa milele, Mfalme wa amani.
7. Maongeo ya enzi yake na amaniHayatakuwa na mwisho kamwe,Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake;Kuuthibitisha na kuutegemezaKwa hukumu na kwa haki,Tangu sasa na hata milele.Wivu wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo.
8. Bwana alimpelekea Yakobo neno, likamfikilia Israeli.
9. Nao watu wote watajua, yaani, Efraimu na yeye akaaye Samaria, wasemao kwa kiburi na kwa kujisifu nafsi zao,
10. Matofali yameanguka, lakini sisi tutajenga kwa mawe yaliyochongwa; mikuyu imekatwa lakini sisi tutaweka mierezi badala yake.
11. Kwa sababu hiyo BWANA atawainua adui wa Resini juu yake, naye atawachochea adui zake;
12. Waashuri upande wa mbele, na Wafilisti upande wa nyuma, nao watamla Israeli kwa kinywa kilicho wazi. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.
13. Lakini watu hao hawakumwelekea yeye aliyewapiga, wala kumtafuta BWANA wa majeshi.