Imbeni, enyi mbingu; ufurahi, Ee nchi;Pazeni sauti ya kuimba, enyi milima;Kwa kuwa BWANA amewafariji watu wake,Naye atawahurumia watu wake walioteswa.