1. Haya, shuka, keti mavumbini,Ewe bikira, binti Babeli;Keti chini pasipo kiti cha enzi,Ewe binti wa Wakaldayo;Maana hutaitwa tena mwororo, mpenda anasa.
2. Twaa mawe ya kusagia, usage unga;Vua utaji wako, ondoa mavazi yako,Funua mguu wako, pita katika mito ya maji.
3. Uchi wako utafunuliwa,Naam, aibu yako itaonekana.Nitalipa kisasi; simkubali mtu ye yote.
4. Mkombozi wetu, BWANA wa majeshi ndilo jina lake,Mtakatifu wa Israeli.
5. Kaa kimya, ingia gizani,Ee binti wa Wakaldayo;Maana hutaitwa tena Malkia wa falme.
6. Nalikuwa nimekasirika na watu wangu, naliutia unajisi urithi wangu, nikawatia mkononi mwako; wewe hukuwatendea rehema; uliwatia wazee nira yako, nayo nzito sana.
7. Ukasema, Mimi nitakuwa bibi milele; hata hukuyatia hayo moyoni mwako, wala hukukumbuka mwisho wa mambo hayo.