Imbeni, enyi mbingu, maana BWANA ametenda hayo;Pigeni kelele, enyi mabonde ya nchi;Pazeni nyimbo, enyi milima;Nawe, msitu, na kila mti ndani yake.Maana BWANA amemkomboa Yakobo,Naye atajitukuza katika Israeli.