2. Hatalia, wala hatapaza sauti yake, wala kuifanya isikiwe katika njia kuu.
3. Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi utokao moshi hatauzima; atatokeza hukumu kwa kweli.
4. Hatazimia, wala hatakata tamaa, hata atakapoweka hukumu duniani; na visiwa vitaingojea sheria yake.
5. Mungu BWANA anena, yeye aliyeziumba mbingu, na kuzitanda; yeye aliyeitandaza nchi na mazao yake; yeye awapaye pumzi watu walio juu yake; yeye awapaye roho wao waendao ndani yake.
6. Mimi, BWANA, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa;
7. kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa.
8. Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu.
9. Tazama, mambo ya kwanza yamekuwa, nami nayahubiri mambo mapya; kabla hayajatokea nawapasheni habari zake.
10. Mwimbieni BWANA wimbo mpya,Na sifa zake tokea mwisho wa dunia;Ninyi mshukao baharini, na vyote vilivyomo,Na visiwa, nao wakaao humo.
11. Jangwa na miji yake na ipaze sauti zao,Vijiji vinavyokaliwa na Kedari;Na waimbe wenyeji wa Sela,Wapige kelele toka vilele vya milima.
12. Na wamtukuze BWANA,Na kutangaza sifa zake visiwani.
13. BWANA atatokea kama shujaa;Ataamsha wivu kama mtu wa vita;Atalia, naam, atapiga kelele;Atawatenda adui zake mambo makuu.
14. Siku nyingi nimenyamaza kimya; nimenyamaza, nikajizuia; sasa nitapiga kelele kama mwanamke aliye katika kuzaa; nitaugua na kutweta pamoja.