18. Sikilizeni, enyi viziwi; tazameni, enyi vipofu, mpate kuona.
19. Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu? Au aliye kiziwi, kama mjumbe wangu nimtumaye? Ni nani aliye kipofu, kama yeye aliye na amani? Naam, kipofu kama mtumishi wa BWANA?
20. Unaona mambo mengi, lakini huyatii moyoni; masikio yake ya wazi, lakini hasikii.
21. BWANA akapendezwa, kwa ajili ya haki yake, kuitukuza sheria, na kuiadhimisha.
22. Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.
23. Ni nani miongoni mwenu atakayetega sikio lake kuyasikia hayo? Atakayesikiliza na kusikia kwa wakati ujao?
24. Ni nani aliyemtoa Yakobo awe mateka, aliyemtia Israeli katika mikono ya wanyang’anyi? Si yeye, BWANA? Yeye tuliyemkosa, ambaye hawakutaka kwenda katika njia zake, wala hawakuitii sheria yake.
25. Kwa sababu hiyo alimwaga ukali wa hasira yake juu yake, na nguvu za vita; ukawasha moto wa kumzunguka pande zote, wala hakujua; ukamteketeza, wala hakuyatia hayo moyoni mwake.