Isa. 3:18-23 Swahili Union Version (SUV)

18. Siku hiyo BWANA atawaondolea uzuri wa njuga zao, na kaya zao;

19. na pete za masikio, na vikuku, na taji zao;

20. na dusumali, na mafurungu, na vitambi, na vibweta vya marashi, na matalasimu;

21. na pete, na azama,

22. na mavazi ya sikukuu, na debwani; na shali, na vifuko;

23. na vioo vidogo, na kitani nzuri, na vilemba, na utaji.

Isa. 3