10. Waambieni wenye haki ya kuwa watakuwa heri, kwa maana watakula matunda ya matendo yao
11. Ole wake mtu mbaya; shari itakuwa kwake, kwa maana atapewa ijara ya mikono yake.
12. Katika habari za watu wangu, watoto ndio wanaowaonea, na wanawake ndio wanaowatawala. Enyi watu wangu, wakuongozao wakukosesha, waiharibu njia ya mapito yako.
13. BWANA asimama ili atete, asimama ili awahukumu watu.
14. BWANA ataingia katika kuwahukumu wazee wa watu wake na wakuu wao; Ninyi ndinyi mliokula shamba la mizabibu; vitu mlivyowateka maskini vi ndani ya nyumba zenu.