Isa. 27:1-9 Swahili Union Version (SUV)

1. Katika siku hiyo BWANA, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule mwenye kuzonga-zonga; naye atamwua yule joka aliye baharini.

2. Katika siku hiyo; Shamba la mizabibu la mvinyo, liimbieni.

3. Mimi, BWANA, nalilinda,Nitalitia maji kila dakika,Asije mtu akaliharibu;Usiku na mchana nitalilinda.

4. Hasira sinayo ndani yangu;Kama mibigili na miiba ingekuwa mbele zangu,Ningepanga vita juu yake,Ningeiteketeza yote pamoja.

5. Au azishike nguvu zangu,Afanye amani nami;Naam, afanye amani nami.

6. Siku zijazo Yakobo atatia mizizi;Israeli atatoa maua na kuchipuka;Nao watajaza uso wa ulimwengu matunda.

7. Je! Amempiga kama hilo pigo la hao waliompiga, au ameuawa kama walivyouawa wao waliouawa na yeye?

8. Umemwadhibu kwa kiasi, ulipomfukuza; ukampepeta kwa upepo mkali katika siku ya upepo wa mashariki.

9. Basi, uovu wa Yakobo utatakaswa hivyo, na hayo ndiyo matunda yote ya kumwondolea dhambi yake; afanyapo mawe yote ya madhabahu kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa, hata maashera na sanamu za jua havitasimama tena.

Isa. 27