4. Mtumainini BWANA siku zoteMaana BWANA YEHOVA ni mwamba wa milele.
5. Kwa kuwa amewashusha wakaao juu,Mji ule ulioinuka, aushusha,Aushusha hata nchi, auleta hata mavumbini.
6. Mguu utaukanyaga chini,Naam, miguu yao walio maskini,Na hatua zao walio wahitaji.
7. Njia yake mwenye haki ni unyofu;Wewe uliye mnyofu wainyosha njia ya mwenye haki.
8. Naam, katika njia ya hukumu zakoSisi tumekungoja, Ee BWANA;Shauku ya nafsi zetu inaelekeaJina lako na ukumbusho wako.
9. Kwa nafsi yangu nimekutamani wakati wa usiku;Naam, kwa nafsi yangu ndani yangu nitakutafuta mapema;Maana hukumu zako zikiwapo duniani,Watu wakaao duniani hujifunza haki.
10. Mtu mbaya ajapofadhiliwa,Hata hivyo hatajifunza haki;Katika nchi ya unyofu atatenda udhalimu,Wala hatauona utukufu wa BWANA.