2. Wekeni wazi malango yake,Taifa lenye haki, lishikalo kweli, liingie.
3. Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemeaKatika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.
4. Mtumainini BWANA siku zoteMaana BWANA YEHOVA ni mwamba wa milele.
5. Kwa kuwa amewashusha wakaao juu,Mji ule ulioinuka, aushusha,Aushusha hata nchi, auleta hata mavumbini.
6. Mguu utaukanyaga chini,Naam, miguu yao walio maskini,Na hatua zao walio wahitaji.
7. Njia yake mwenye haki ni unyofu;Wewe uliye mnyofu wainyosha njia ya mwenye haki.
8. Naam, katika njia ya hukumu zakoSisi tumekungoja, Ee BWANA;Shauku ya nafsi zetu inaelekeaJina lako na ukumbusho wako.
9. Kwa nafsi yangu nimekutamani wakati wa usiku;Naam, kwa nafsi yangu ndani yangu nitakutafuta mapema;Maana hukumu zako zikiwapo duniani,Watu wakaao duniani hujifunza haki.
10. Mtu mbaya ajapofadhiliwa,Hata hivyo hatajifunza haki;Katika nchi ya unyofu atatenda udhalimu,Wala hatauona utukufu wa BWANA.
11. BWANA, mkono wako umeinuliwa, lakini hawaoni; lakini watauona wivu wako kwa ajili ya watu wako, nao watatahayari; naam, moto utawala adui zako.
12. BWANA, utatuamuria amani; maana ni wewe pia uliyetutendea kazi zetu zote.
13. Ee BWANA, Mungu wetu, mabwana wengine zaidi ya wewe wametumiliki; lakini kwa msaada wako peke yako tutalitaja jina lako.
14. Wao wamekufa, hawataishi; wamekwisha kufariki, hawatafufuka; kwa sababu hiyo umewajilia, na kuwaangamiza, na kuupoteza ukumbusho wao.
15. Umeliongeza hilo taifa, BWANA, umeliongeza taifa; wewe umetukuzwa, umeipanua mipaka yote ya nchi hii.