Isa. 19:5-7 Swahili Union Version (SUV)

5. Na maji ya baharini yatapunguka, na huo mto utakauka na kuwa pakavu.

6. Na vijito vya mto vitatoa uvundo, na mifereji ya Misri itakuwa haina maji mengi, itakauka; manyasi na mianzi itanyauka.

7. Vitu vimeavyo karibu na Nile, katika ukingo wa Nile, na vyote vilivyopandwa karibu na Nile vitakauka na kuondolewa na kutoweka.

Isa. 19