2. Miji ya Aroeri imeachwa; itakuwa kwa makundi ya kondoo, nao watajilaza huko wala hapana atakayewatia hofu.
3. Na ngome ya Efraimu itakomeshwa, na ufalme wa Dameski, na mabaki ya Shamu; watakuwa kama utukufu wa wana wa Israeli, asema BWANA wa majeshi.
4. Tena itakuwa katika siku hiyo, utukufu wa Yakobo utapungua-pungua, na kunona kwa mwili wake kutakonda.
5. Tena itakuwa kama hapo avunaye ashikapo mabua ya ngano, na mkono wake ukatapo masuke; tena itakuwa kama hapo mtu aokotapo masuke katika bonde la Warefai.
6. Lakini kilichosazwa na mvunaji kitakuwa ndani yake, kama vile wakati wa kupiga mizeituni, matunda mawili matatu yaliyo juu sana; matunda manne matano katika matawi, matawi ya mti wa matunda, asema BWANA, Mungu wa Israeli.