5. BWANA amelivunja gongo la wabaya,Fimbo ya enzi yao wenye kutawala.
6. Yeye aliyewapiga mataifa kwa ghadhabu,Kwa mapigo yasiyokoma;Aliyewatawala mataifa kwa hasira,Ameadhibiwa asizuie mtu.
7. Dunia yote inastarehe na kutulia;Hata huanzilisha kuimba.
8. Naam, misunobari inakufurahia,Na mierezi ya Lebanoni, ikisema,Tokea wakati ulipolazwa chini wewe,Hapana mkata miti aliyetujia.
9. Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili yako,Ili kukulaki utakapokuja;Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako,Naam, walio wakuu wote wa dunia;Huwainua wafalme wote wa mataifa,Watoke katika viti vyao vya enzi.
10. Hao wote watajibu na kukuambia,Je! Wewe nawe umekuwa dhaifu kama sisi!Wewe nawe umekuwa kama sisi!