4. Ee Efraimu, nikutendee nini? Ee Yuda, nikutendee nini? Kwa maana fadhili zenu ni kama wingu la asubuhi na kama umande utowekao mapema.
5. Kwa sababu hiyo nimewakata-kata kwa vinywa vya manabii; nimewaua kwa maneno ya kinywa changu; na hukumu yangu itatokea kama mwanga.
6. Maana nataka fadhili wala si sadaka; na kumjua Mungu kuliko sadaka za kuteketezwa.
7. Lakini wao wamelivunja hilo agano kama Adamu; huko wamenitenda mambo ya hiana.
8. Gileadi ni mji wa hao watendao maovu, umetiwa rangi ya damu.