Hos. 5:5-11 Swahili Union Version (SUV)

5. Na kiburi cha Israeli chamshuhudia mbele ya uso wake; kwa sababu hiyo, Israeli na Efraimu watajikwaa katika uovu wao. Yuda naye atajikwaa pamoja nao.

6. Watakwenda na makundi yao ya kondoo na ng’ombe wamtafute BWANA; lakini hawatamwona; amejitenga nao.

7. Wametenda kwa hila juu ya BWANA; maana wamezaa wana wageni; sasa mwezi huu uandamao utawala pamoja na mashamba yao.

8. Pigeni tarumbeta katika Gibea, na baragumu katika Rama; pazeni sauti ya hofu katika Beth-Aveni; nyuma yako, Ee Benyamini!

9. Efraimu atakuwa ukiwa siku ya kukemewa; katika kabila za Israeli nimetangaza habari itakayotokea halafu bila shaka.

10. Wakuu wa Yuda ni kama watu waondoao alama ya mpaka; nitawamwagia ghadhabu yangu kama maji.

11. Efraimu ameonewa, amesetwa katika hukumu, kwa sababu alikuwa radhi kufuata ubatili.

Hos. 5