Hos. 5:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Sikieni haya, enyi makuhani, sikilizeni, enyi nyumba ya Israeli, tegeni masikio yenu, enyi wa nyumba ya mfalme, kwa kuwa hukumu hii yawahusu ninyi; maana mmekuwa mtego huko Mizpa, na wavu uliotandwa juu ya Tabori.

2. Nao walioasi wameongeza sana ufisadi wao; lakini mimi ndiye awakaripiaye wote pia.

3. Mimi namjua Efraimu, wala Israeli hakufichwa nisimwone; maana sasa, Ee Efraimu, umefanya uzinzi; Israeli ametiwa unajisi.

Hos. 5