11. Nimekupa mfalme katika hasira yangu, nikamwondoa katika ghadhabu yangu.
12. Uovu wa Efraimu umefungwa kwa kukazwa; dhambi yake imewekwa akiba.
13. Utungu wa mwanamke mwenye mimba utampata; yeye ni mwana asiye na akili; maana wakati umewadia, ambao haimpasi kukawia mahali wapenyapo watoto.