10. Tena nimenena na hao manabii, nami nimeongeza maono, na kwa utumishi wa manabii nimetumia mifano.
11. Je! Gileadi ni uovu? Wamekuwa ubatili tu; huko Gilgali hutoa dhabihu za ng’ombe; naam, madhabahu zao zimekuwa kama chungu katika matuta ya mashamba.
12. Na Yakobo alikimbia mpaka Padan-Aramu,Na Israeli alitumika apate mke;Ili apate mke alichunga kondoo.
13. Na kwa nabii BWANA alimtoa Israeli katika Misri,Na kwa mkono wa nabii alihifadhiwa.
14. Efraimu amenitia hasira kali sana; kwa sababu hiyo damu yake itaachwa juu yake, na Bwana wake atamrudishia lawama yake.