1. Efraimu hujilisha upepo, na kuandamana na upepo wa mashariki; haachi kuongeza uongo na uharibifu; nao wafanya agano na Ashuru, na mafuta huchukuliwa kwenda Misri.
2. BWANA naye ana mateto na Yuda, naye atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake; kwa kadiri ya matendo yake atamlipa.
3. Tumboni alimshika ndugu yake kisigino;Na alipokuwa mtu mzima alikuwa na uwezo kwa Mungu;
4. Naam, alikuwa na uwezo juu ya malaikaAkashinda; alilia, na kumsihi;Alimwona huko Betheli, naye akasema nasi huko;
5. Naam, BWANA, Mungu wa majeshi;BWANA ndilo kumbukumbu lake.
6. Basi, mrudie Mungu wako; shika fadhili na hukumu; ukamngojee Mungu wako daima.
7. Ni mchuuzi, mizani ya udanganyifu i mkononi mwake; anapenda kudhulumu.
8. Naye Efraimu alisema, Kweli nimekuwa tajiri, nimejipatia mali nyingi; katika kazi zangu zote hawataona kwangu uovu wo wote uliokuwa dhambi.
9. Lakini mimi ni BWANA, Mungu wako tangu ulipotoka katika nchi ya Misri; nitakukalisha tena katika hema, kama siku za karamu ya idi.