1. Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
2. Nena na Haruni, ukamwambie, Utakapoziweka taa, hizo taa saba zitatoa nuru hapo mbele ya kinara cha taa.
3. Basi Haruni akafanya; akaziweka taa zake ili zitoe nuru hapo mbele ya kinara, kama BWANA alivyomwagiza Musa.
4. Na hii ndiyo kazi ya hicho kinara cha taa, ilikuwa ni kazi ya ufuzi wa dhahabu; tangu tako lake hata maua yake kilikuwa ni kazi ya ufuzi; vile vile kama ule mfano BWANA aliokuwa amemwonyesha Musa, ndivyo alivyokifanya kinara.