Hes. 7:80-85 Swahili Union Version (SUV)

80. na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba;

81. na ng’ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa;

82. na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;

83. tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng’ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Ahira mwana wa Enani.

84. Hayo ndiyo matoleo yaliyotolewa na wakuu wa Israeli kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu, siku hiyo ilipotiwa mafuta; sahani za fedha kumi na mbili, na bakuli za fedha kumi na mbili, na vijiko vya dhahabu kumi na viwili;

85. kila sahani ya fedha uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na kila bakuli uzani wake ni shekeli sabini; fedha yote ya vile vyombo ilikuwa shekeli elfu mbili na mia nne, kwa shekeli ya mahali patakatifu;

Hes. 7