Hes. 7:61-74 Swahili Union Version (SUV)

61. matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga;

62. na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba;

63. na ng’ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa;

64. na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;

65. tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng’ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Abidani mwana wa Gideoni.

66. Siku ya kumi Ahiezeri mwana wa Amishadai, mkuu wa wana wa Dani;

67. matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga;

68. na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba;

69. na ng’ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa;

70. na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;

71. tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng’ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Ahiezeri mwana wa Amishadai.

72. Na siku ya kumi na moja Pagieli mwana wa Okrani, mkuu wa wana wa Asheri;

73. matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga;

74. na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba;

Hes. 7