22. na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;
23. na kwa dhabihu ya sadaka za amani, ng’ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Nethaneli mwana wa Suari.
24. Siku ya tatu Eliabu mwana wa Heloni, mkuu wa wana wa Zabuloni;
25. matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga;
26. na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba;
27. na ng’ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa;
28. na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;
29. tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng’ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Eliabu mwana wa Heloni.
30. Siku ya nne Elisuri mwana wa Shedeuri, mkuu wa wana wa Reubeni;