29. Hii ndiyo sheria ya wivu, mwanamke, ambaye yu chini ya mumewe, akikengeuka, na kupata unajisi;
30. au, roho ya wivu ikimwingia mtu mume, naye akamwonea wivu mkewe; ndipo atakapomweka huyo mwanamke mbele za BWANA, na kuhani atatenda juu yake sheria hii yote.
31. Na huyo mume atakuwa hana uovu, na mwanamke atauchukua uovu wake.