1. Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
2. Waamrishe wana wa Israeli kwamba wamtoe kila mwenye ukoma maragoni, na kila mtu aliye na kisonono, na kila aliye najisi kwa ajili ya wafu;
3. mtawatoa nje wote, waume kwa wake, mtawaweka nje ya marago; ili wasiyatie unajisi marago yao, ambayo mimi naketi katikati yake.
4. Wana wa Israeli wakafanya vivyo, wakawatoa na kuwaweka nje ya marago; kama BWANA alivyonena na Musa, ndivyo walivyofanya wana wa Israeli.
5. Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,