Hes. 34:17-29 Swahili Union Version (SUV)

17. Haya ndiyo majina ya watu watakaowagawanyia nchi iwe urithi wenu; Eleazari kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni.

18. Kisha mtamtwaa mkuu mmoja wa kila kabila, ili waigawanye nchi iwe urithi wenu.

19. Na majina ya watu hao ni haya; katika kabila ya Yuda, ni Kalebu mwana wa Yefune.

20. Na katika kabila ya wana wa Simeoni, Shemueli mwana wa Amihudi.

21. Katika kabila ya Benyamini, ni Elidadi mwana wa Kisloni.

22. Na katika kabila ya wana wa Dani, mkuu, Buki mwana wa Yogli.

23. Katika wana wa Yusufu; katika kabila ya wana wa Manase, mkuu, Hanieli mwana wa Efodi;

24. na katika kabila ya wana wa Efraimu, mkuu, Kemueli mwana wa Shiftani.

25. Na katika kabila ya wana wa Zabuloni, mkuu, Elisafani mwana wa Parnaki.

26. Na katika kabila ya wana wa Isakari, mkuu, Paltieli mwana wa Azani.

27. Na katika kabila ya wana wa Asheri, mkuu, Ahihudi mwana wa Shelomi.

28. Na katika kabila ya wana wa Naftali, mkuu, Pedaheli mwana wa Amihudi.

29. Hao ndio BWANA aliowaagiza wawagawanyie urithi wana wa Israeli katika nchi ya Kanaani.

Hes. 34