Hes. 34:14-24 Swahili Union Version (SUV)

14. kwa kuwa kabila ya wana wa Reubeni kwa nyumba za baba zao, na kabila ya wana wa Gadi kwa nyumba za baba zao, wamekwisha pata, na hiyo nusu ya kabila ya Manase wamekwisha pata urithi wao;

15. hizo kabila mbili na nusu ya kabila wamekwisha pata urithi wao huko ng’ambo ya pili ya Yordani, hapo Yeriko, upande wa mashariki, kuelekea maawio ya jua.

16. Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,

17. Haya ndiyo majina ya watu watakaowagawanyia nchi iwe urithi wenu; Eleazari kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni.

18. Kisha mtamtwaa mkuu mmoja wa kila kabila, ili waigawanye nchi iwe urithi wenu.

19. Na majina ya watu hao ni haya; katika kabila ya Yuda, ni Kalebu mwana wa Yefune.

20. Na katika kabila ya wana wa Simeoni, Shemueli mwana wa Amihudi.

21. Katika kabila ya Benyamini, ni Elidadi mwana wa Kisloni.

22. Na katika kabila ya wana wa Dani, mkuu, Buki mwana wa Yogli.

23. Katika wana wa Yusufu; katika kabila ya wana wa Manase, mkuu, Hanieli mwana wa Efodi;

24. na katika kabila ya wana wa Efraimu, mkuu, Kemueli mwana wa Shiftani.

Hes. 34