11. kisha mpaka utatelemka kutoka Shefamu mpaka Ribla, upande wa mashariki wa Aini; kisha mpaka utatelemka na kufikilia upande wa bahari ya Kinerethi upande wa mashariki;
12. kisha mpaka utatelemkia Yordani, na kutokea kwake kutakuwa hapo katika Bahari ya Chumvi; hii ndiyo nchi yenu kama mipaka yake ilivyo kuizunguka pande zote.
13. Kisha Musa akawaagiza wana wa Israeli, akisema, Hii ndiyo nchi mtakayoirithi kwa kupiga kura, ambayo BWANA ameagiza wapewe watu wa zile kabila kenda, na nusu ya kabila;
14. kwa kuwa kabila ya wana wa Reubeni kwa nyumba za baba zao, na kabila ya wana wa Gadi kwa nyumba za baba zao, wamekwisha pata, na hiyo nusu ya kabila ya Manase wamekwisha pata urithi wao;
15. hizo kabila mbili na nusu ya kabila wamekwisha pata urithi wao huko ng’ambo ya pili ya Yordani, hapo Yeriko, upande wa mashariki, kuelekea maawio ya jua.
16. Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
17. Haya ndiyo majina ya watu watakaowagawanyia nchi iwe urithi wenu; Eleazari kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni.
18. Kisha mtamtwaa mkuu mmoja wa kila kabila, ili waigawanye nchi iwe urithi wenu.
19. Na majina ya watu hao ni haya; katika kabila ya Yuda, ni Kalebu mwana wa Yefune.
20. Na katika kabila ya wana wa Simeoni, Shemueli mwana wa Amihudi.
21. Katika kabila ya Benyamini, ni Elidadi mwana wa Kisloni.
22. Na katika kabila ya wana wa Dani, mkuu, Buki mwana wa Yogli.
23. Katika wana wa Yusufu; katika kabila ya wana wa Manase, mkuu, Hanieli mwana wa Efodi;