38. Haruni akakwea mlima wa Hori, kwa amri ya BWANA, akafa hapo, katika mwaka wa arobaini baada ya wana wa Israeli kutoka katika nchi ya Misri, mwezi wa tano, siku ya kwanza ya mwezi.
39. Naye Haruni alikuwa mtu wa umri wa miaka mia na ishirini na mitatu hapo alipokufa katika mlima wa Hori.
40. Ndipo Mkanaani, mfalme wa Aradi, aliyekaa pande za Negebu katika nchi ya Kanaani akasikia habari za kuja kwao wana wa Israeli.
41. Nao wakasafiri kutoka mlima wa Hori, wakapanga Salmona.
42. Wakasafiri kutoka Salmona, wakapanga Punoni.
43. Wakasafiri kutoka Punoni, wakapanga Obothi.
44. Wakasafiri kutoka Obothi, wakapanga Iye-abarimu, katika mpaka wa Moabu.
45. Wakasafiri kutoka Iye-abarimu, wakapanga Dibon-gadi.
46. Wakasafiri kutoka Dibon-gadi, wakapanga Almon-diblathaimu.